Tuesday 14 July 2015

SEMINA ILIFANYIKA MPWAPWA KIJIJI CHA MBORI 04/07-12/07/2015

Kichwa cha somo:-  JIFUNZE KUTENGENEZA MAZINGIRA ILI UPATE MSAADA WA MUNGU KATIKA HALI ZOTE


Mch Pearson Nhayo akiongoza semina hiyo


Wanaume na wanawake wengi walihudhulia

Baadhi ya watu waliohudhulia Semina

 Katika somo hilo lililotoka kwenye kirtabu cha ISAYA 6:5 linasema "Ndipo niliposema, Ole wangu kwa maana nimepotea, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye midomo michafu nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu na macho yangu yamemuona mfalme, Bwana wa Majeshi. "Na lilikuwa na mfululizo ufuatao:

1. Utangulizi. Yapo Mazingira kama ya Isaya kwa Wakristo Wengi yanayomzuia Mungu asikusaidie
2. Mifano ya mazingira yanayoweza kumsababisha Mungu asiingilielie kati Maisha yako
-Mazingira ya Kidini,
-yahali ya kinafsi,
-ya ardhi,
-ya anga,
-ya kuzaliwa,
-ya kiumli ya kiroho,
-ya kijamii,
-ya kiuongozi
n.k
Kuna Mambo ukiyafanya, unakuwa umeweka agano na mauti, umepatana na kuzimu na hivyo lazima utengeneze hayo mazingira ili Mungu aingilie kati maisha yako.
 3. Unawezaje kujua kuwa yapo mazingira yanapaswa kutengenezwa? Kama unatabia zifuatazo utajua tu!!!!
-Huzuni isiyo kifani,
-Unakuwa na mabadiliko ya polepole sana
-Unakuwa na hasira inayokwenda kwenye chuki
-unamtegemea sana binadamu kuliko Mungu
n.k

4.Kabla ya kuanza kutengeneza mazingira inapaswa ujue yafuatayo;-
-Kazi aqlizofanya Yesu msalabani,
-Mamlaka aliyopewa mtu aliyeokoka au kanisa
 -Nguvu ya agano jipya la  kwenye Yeremia

5.Mambo ya kufanya katika kutengeneza Mazingira:
kv kuokoka, kutafakari neno la Mungu, Kuombea ardhi, kuombea Anga, Kufanya maombi ya toba kwa ajili ya FAMILIA YAKO,  usilipize kisasi n.k.

6.Hitimisho. Kuendelea kumtegemea Mungu siku zote.
Mungu akubariki kwa maombi yako yaliyofanikisha semina hii kufanyika na kutimiza kusudi la Mungu. Amen!





No comments:

Post a Comment

Welcome