Friday, 29 August 2014


 UKWATA IRINGA...WILAYA © KILOLO
Yafuatayo ni matukio yalijili katika Joinmass ya UKWATA iliyofanika 25-27/07/2014. Wana UKWATA wengi ambao walikusanyika katika shule ya ST Michael iliypo wilaya ya Kilolo.

Baadhi ya wana ukwata wakisikilza neno la Mungu


Kulikuwa na masomo mbalimbali yakifundishwa na watumishi vijana. Masomo hayo ni pamoja na:-


Somo la kwanza
UHUSIANO ULIOPO KATI YA IMANI NA MAFANIKIO YAKO.

Mwl. Clement Mkuchu

Somo hili lilifundiswa na Mwl. Clement Mkuchu ambaye kwa taaluma ni Tabibu katika Kituo cha Afya Ismani-Iringa. Katika somo hilo Mw Mkuchu alisema hivi na hapa namnukuu:-
Mafanikio maana yake ni kukua tka kiwango cha chini kwenda juu. Na kuna uhusiano kati ya Imani ya mtu aliyonayo juu ya Mungu na Mafanikio yake.
Ukisoma Waebrania 11:1 Inasema imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Basi imani ni tarajio. Hiyo nguvu ya kile unachotarajia ipo kwenye uwazi au bayana. Na ile nguvu ya kutarajia kitu kisichoonekana, ndiyo inaitwa mafanikio. Mkuchu aliendelea kuwaeleza wanaukwata na ambao ni wanafunzi wa sekondari kutoka shule mbalimbali kwamba, Mtu anaweza kuwa na uhakika wa kupata division one kabla ya kufanya mtihani wake wa mwisho kuhitimu masomo yake. Aliendelea kusema kuwa ndani ya Imani kuna mambo yafuatayo:-
  1. Kunena au kutamka au kukiri kile unachokitarajia kabla hakijatokea 2Wakorintho 4:13.
  2. Pia imani inakupa picha ya kile unachokitarajia juu ya maisha yako ya sasa na baadae. Kwa mfano, Kama ndani yako picha ya kuwa Daktari, au Mwalimu au Mwanasheri au Mhandisi, basinutaweza kuona hilo jambo ndani yako.
  3. Kuna mazingira ya ki-Mungu, yanayoweza kukusaidia kutembea sawasawa na kile unachokiamini.
Alisema mambo mengi, lakini kwa ujumla aliwahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii, maana kama wamempa Yesu maisha yao ni muhimu wawe vichwa wala sio mkia. Alijitolea mfano mwenyewe kuwa, alipofanya mtihani wa kwanza wa somo la Physics ,akiwa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Mzumbe, alipata alama 34%. Na alipoendelea kujisomea kwa bidii alipata alama 84% katika mtihani uliofuta. Pia aliwapa changamoto wana UKWATA, ya kupenda kusoma masomo ya sayansi maana ndiyo yenye fursa nyingi kwa sasa.



Somo la pili.
NGUVU INAYOPATIKANA KWENYE MAOMBI.
Smo hili lilifundishwa na Mwl. Mjuni Kishi, ambaye ni Mwlimu kitaaluma, katika shule ya sekondari Pomerini.
Mwl Mjune akiwa na Mke wake


Kwa jumla Mwl Mjuni aliwahimiza wana UKWATA  kuombea masomo na maisha yao; kwa kuwa mwongozo na nguvuya kuendelea mbele kimaisha inategemea sana maombi.
Kwa upande mwngine, Mjuni akizungumza na mtandao huu, alisema na kushauri kuwa; ni vyema kila aliyeitwa na Mungu kuanza kumtumikia mahali alipo. Na hapa namnukuu;
 "Kuna tofauti ya kumpenda Yesu na Kupendwa na Yesu. Petro alimpenda sana Yesu. Lakini Yohana alipendwa sana na Yesu. Na kwa kuwa Petro alimpenda sana Yesu; ndiyo maana alikabidhiwa kanisa alilishe chakula. Kwa upande wa Yohana, kule kupendwa kwake sana na Yesu kulitengeneza mazingira ya Yohana kubweteka, na hivyo hakupewa kanisa."
Hivyo mwl. Mjuni alisisitiza kuwa watu wampende Yesu ili awatumie kuvuna shambani mwake.



Somo la tatu
Somo lingine lilitolewa Mama Mch. Kinganga. Katika Somo lake alisoma katika kitabu cha 1Samueli 1:1-18. Alisema kuwa Penina na Elikana hawakuwa na unafuu kwa Hana. Wote wawili walikuwa wanataka kumpotezea mweleo wa ki-Mungu Hana. Penina alimsema vibaya Hana. Naa Elikana alimfariji Hana. Lakini faraja ya Elikana ilikusudia kumkatisha moyo wa maombi wa Hana. Lakini Hana aliendelea kuomba sawasawa na Haja ya moyo wake, na Mungu akampatia mtoto aliyeitwa Samueli.
Kwa ujumla mama Mch. Kinganga aliwambia wanafunzi kuwa, Usikubali kufarijika mpaka upate ulichokikusudia. Hata kama familia ya hakuna aliyepiga hatua kimasomo, bado ipo nafasi ya wewe (wanafunzi hao kuvuka mipaka ambayo iblisi ameweka katika ulimwengu wa Roho). Kitu cha muhimu tu ni kutokatatamaa na kumwomba Mungu anayeweza kuvunja nira zote.

Mama Mch. Kinganga wa Iringa


KWAYA ZILIZOSHIRIKI
Baadhi ya Kwaya zilizoshiriki katika Join mass hiyo ni pamoja na:-
  1. Angaza band toka Pomerini-Kilolo.
  2. Mwimbaji Binafsi anayeitwa AUSWELL GOODSON SANGA 
    toka Dar es Salaam. 

    Auswell Goodson Sanga, akiimba wakati wa Jointmass ya UKWATA

No comments:

Post a Comment

Welcome