Tuesday, 26 January 2016

ABOUT ST. MICHAEL SECONDARY SCHOOL-IRINGA TANZANIA(S.1684)

WATU WENGI HAWAJUI KUWA NI MOJA KATI YA SHULE NZURI MKOANI IRINGA (S.1684)
 
St. Michael sekondari-Iringa Jengo la utawala
Wanafunzi wakifurahi kuwepo shuleni St. Michael sekondari

Pia kuna matanki ya kutosha kuvunia maji ya kutumia wakati maji yanakatika.
Watu wengi hawajui kuwa St. Michael sekondari ni moja kati ya shule nzuri kabisa mkoani Iringa na nchini Tanzania kwa ujumla. Ipo wiyani Kilolo, kilometa 35 kutoka Iringa mjini na karibu na barabara kuu itokayo Iringa kwenda Kidabaga.

Shule hiyo ya St. Michael inamilikiwa na kuendeshwa na kanisa la Anglican Dayosisi ya Ruaha. Mazingira yake ni tulivu kwa Mwanafunzi na kuna walimu wa kutosha na wenye uzoefu. 


Kuhusu Maktaba ya shule.

Ina maktaba nzuri na ya kisasa na vitabu vya kutosha kama inavyooshesha hapa chini, ambapo Madam Alice Mlongaa ambaye ndiye libraian wa shule akiwaandikisha wanafunzi kabla ya kuingia ndani ya maktaba kujisomea.









Kuhusu maabara ya shule

Shule hiyo pia ina maabara za kutosha kwa masomo ya sayansi ya Biology, Chemistry na Physics, ambapo wanafunzi hufanya masomo kwa vitendo. Angalia baadhi ya wanafunzi wakifanya mazoezi kwenye maabara hizo.








Karibu sana St. Michael sekondari kwa malezi bora ya mwanao.....piga simu 0764867242 kwa mawasiliano